UNMAS yalaani mashambulizi dhidi ya timu wategua mabomu

27 Januari 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia huduma za kutegua mabomu ya kutegwa ardhini UNMAS limelaani vikali shambulio katika jimbo la Helmand nchini Afghanistan lililolenga timu ya kudhibiti mabomu ya kutegwa ardhini nchini humo DAFA.

Taarifa ya UNMAS imesema kuwa shambulio hilo pia lilielekezwa kwa asasi isiyo ya kiserikali ya udhibiti wa mabomu ya kutegwa ardhini pamoja na wadau wa mpango wa operesheni ya kung’oa mabomu ya kutegwa ardhini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kiongozi wa kijamii wa DAFA hajulikani alipo na kwamba haijulikani hasa nia ya washambuliaji wa wahudumu hao.

UNMAS imeeleza kuwa timu ya DAFA ilikuwa katika kazi  zao za kawadia za kuondoa maabomu ya kutegwa ardhini wakati watu waisojulikana waliojihami kwa silaha walipowasili na kuwashambulia.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter