Uelewa wachochea matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania

27 Januari 2016

Wakati mkutano wa kimataifa kuhusu uzazi wa mpango ukiendelea huko Indonesia, Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) nchini Tanzania limesema uelewa wa faida za matumizi ya njia hizo ni moja ya sababu ya matumizi kuongezeka hadi asilimia 27 huku matarajio ikiwa ni kufikia asilimia 80 mwaka 2020.

Akihojiwa na idhaa hii, afisa programu wa afya ya mama na mtoto UNFPA Tanzania Felister Bwana amesema kiwango cha uelewa ni asilimia 90 na kwamba..

(Sauti ya Felister)

Amesema njia inayotumiwa zaidi na wanawake ni sindano na vipandikizi na kwa wanaume ni mpira wa kiume  na kwamba mteja anaelimishwa na kushauriwa….

(Sauti ya Felister)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter