Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kesi dhidi ya Gbagbo kuanza kesho kwenye mahakama ya ICC

Kesi dhidi ya Gbagbo kuanza kesho kwenye mahakama ya ICC

Kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa Côte d'Ivoire, Laurent Gbagbo itaanza hapo kesho Januari 28, 2016, kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo, Fatou Bensouda. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Laurent Gbagbo, ambaye ni rais wa zamani wa Côte d'Ivoire, aliwasilishwa kwenye ICC mnamo Novemba 30, 2011, ambapo alithibitishiwa mashtaka manne ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, yakiwemo mauaji, ubakaji, na vitendo vingine vya kikatili, vikiwa ni jaribio la kuua na utesaji.

Akitangaza kufunguliwa kwa mashtaka dhidi ya Gbagbo mbele ya wanahabari jijini The Hague, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda, amesema mashahidi wote wapo tayari, ingawa hawawezi kuwekwa hadharani.

(Sauti ya Bensouda)

Gbagbo anashtakiwa pamoja na Charles Blé Goudé - raia wa Côte d'Ivoire - ambaye anakabiliwa na mashtaka yale yale.