Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukizi ya Holocsoust: ubaguzi wakemewa, Tanzania yaadhimisha

Kumbukizi ya Holocsoust: ubaguzi wakemewa, Tanzania yaadhimisha

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga na manusura wa mauaji ya halaiki ya Holocaust, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kumbukizi hii inadhihirisha kile kinachoweza kutokea iwapo binadamu atasahau utu wao. Taarifa kamili na Flora Nducha..

(TAARIFA YA FLORA)

Katika ujumbe wake Ban amesema mauaji ya Holocaust dhidi ya wayahudi yalikuwa uhalifu mkubwa ambao hadi sasa hakuna mtu anayeweza kupinga kuwa yalitokea na hivyo kumbukizi yake ni hatua ya kurejelea azma ya kuzuia vitendo hivyo visitokee tena.

Nchini Tanzania nako Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umedhimisha kumbukumbu hiyo aleta pamoja wadau wa amani wakwamo wanafunzi kutoka shule mbalimbali za msingi na sekondari, ambapo wameutizama katika video ujumbe wa Ban kuhusu kumbukizi hiyo na kisha.

Nuts!

Ni tamko la pamoja la kupinga mauaji kama hayo kujirudia tena ambapo balozi wa Ujerumani nchini Tanzania John Reyels aliwaongoza wageni hususani wanafunzi kutamka na akasisitiza.

(SAUTI JOHN)

‘‘Tunahitaji kuendelea kusambaza ujumbe kuhusu Holocaust, uhalifu mkubwa uliotendwa na watu wa Ujerumani. Kila mwanafunzi duniani anapswa kufahamu. Kwasababu kila anayefahamu lazima ahisi deni la kusema kamwe yasitokee.’’

Usia Ledama ni afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Tanzania.

(SAUTI USIA)