Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 339 zahitajika kukidhi mahitaji yakibinadamu Afghanistan 2016:OCHA

Dola milioni 339 zahitajika kukidhi mahitaji yakibinadamu Afghanistan 2016:OCHA

Jumuiya ya watoa misaada wa kimataifa kwa pamoja nchini Afghanistan wanatafuta dola milioni 393 ili kukidhi mahitaji ya kuokoa maisha kwa watu wasiojiweza na waliotengwa nchini humo kwa kipindi cha 2016.

Msaada huo unaojumuisha chakula, fursa za afya, lishe, maji safi na kujisafi utawafikia watu takribani milioni 3.5 waliowekwa katika mpngo maalumu wa huduma za kibinadamu wa 2016 nchini Afghanistan.

Kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadmu OCHA Mark Bowden, shirika la OCHA linapongeza juhudi zote za mwaka 2015 lakini anaamini juhudi hizo zinahitaji kuongezwa mara mbili katika miezi 12 ijayo..

Tangu Januari hadi Novemba 2015 watu Zaidi ya 300,000 walilazimika kukimbia makwao nchini Afghanistan kutokana na vita na kufikia ongezeko la asilimia 160 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.