Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa Palestina wana haki ya kukata tamaa: Ban Ki-moon

Raia wa Palestina wana haki ya kukata tamaa: Ban Ki-moon

Leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejadili hali ya Mashariki ya Kati likiwemo suala la Palestina, huku Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwasilisha ripoti yake na kusihi pande zote kwenye mzozo wa eneo hilo kuchukua hatua ili kutoharibu daima uwezekano wa kutekeleza suluhu ya mataifa mawili.

Bwana Ban ameeleza kwamba hakuna dalili ya kupungua kwa mivutano na misimamo mikali, akisikitishwa na ripoti ya mashambulizi dhidi ya raia wa Palestina na Israel.

Amesisitiza kwamba harakati za kiusalama hazitafanikiwa kusitisha ghasia, kwani vijana wa Palestina wamekatishwa tamaa kutokana na kutawaliwa kwa zaidi ya miaka 50 na kukwama kwa mazungumzo ya amani.

Kuhusu vitendo vya Israel kuharibu nyumba za wapalestina na kujenga nyumba za walowezi wa Israel kinyume na sheria Ban amesema..

(Sauti ya Ban)

“ Ili mchakato wa amani ufanikiwe, ni lazima Israel isitishe mpango wake wa kupanua ujenzi huo. Kuendelea na shughuli za upanuzi ni wa makazi hayo ni kuwatusi raia wa Palestina na jamii ya kimataifa. Pia kunaibua mashaka kuhusu utashi wa Israel wa kutekeleza suluhu ya mataifa mawili.”