Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timu ya kuchunguza ukiukaji wa haki Burundi iko tayari, ruksa ndio shida:UM

Timu ya kuchunguza ukiukaji wa haki Burundi iko tayari, ruksa ndio shida:UM

Baraza la Haki za Binadamu limeunda jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kwenda Burundi kuchunguza unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo. Jopo hilo linajumuisha wawakilishi maalumu wawili na mjumbe wa tume ya Afrika kwa ajili ya haki za binadamu. Amina Hassan na taarifa kamili..

(TAARIFA YA AMINA)

Mbali ya kuchunguza uchunguzi jopo hilo lilitatakiwa kutoa mapendekezo ya kuimarisha hali ya haki za binadamu na kushiriki mazungumzo na serikali na wadau wengine muhimu katika mgogoro unaoendelea Burundi.

Kufuatia kuzidi kuzorota kwa hali kamishina mkuu wa haki za binadamu aliiomba serikali ya Burundi kuruhusu jopo hilo kuanza kazi yao Jumatatu 25 Januari lakini amesema hilo limeshidikana na mpango kucheleweshwa kwa sababu serikali ya Burundi haikujibu ombi hilo kama anavyofafanua Cécile Pouilly msemaji wa ofisi ya haki za binadamu..

(SAUTI YA CECILE POUILY)

“Tunahofia kwamba itazuia timu kuweza kutimiza majukumu yake na kuwasilisha ripoti mbele ya Baraza jinsi inavyofaa. Tunatumai mamlaka za Burundi zintachukua hatua zote zinazohitajika ikiwemo kutoa visa, ili kuwezesha wataalam hao kufika nchi humo.”