Skip to main content

Waathirika wa Boko Haramu wanahitaji kujua siyo kosa lao

Waathirika wa Boko Haramu wanahitaji kujua siyo kosa lao

Wanawake na wasichana ambao wamefanyiwa ukatili na kundi la kigaidi la Nigeria la Boko Haram wanahitaji kujua sio kosa lao.

Ujumbe huo ni kutoka kwa mtaalamu wa Umoja wa mataifa ambaye amerejea kutoka ziara ya kutembelea makambi ya wakimbizi wa ndani zilizoko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo ya Afrika.

Mtaalamu huyo ambaye ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa Maud de Boer-Buquicchio, amesema idadi isiyojulikana ya wanawake nchini wanakabiliwa na mtihani wa kuwa mama, huku wote wakitengwa na jamii na hata familia zao wenyewe baada ya kubakwa na wanamgambo wa kundi la waasi la Boko Haram.