Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF na ombi la dola Bilioni 2.8 kukwamua watoto maeneo mbali mbali

UNICEF na ombi la dola Bilioni 2.8 kukwamua watoto maeneo mbali mbali

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limezindua ombi la dola Bilioni 2.8 kwa ajili ya kufikia watoto Milioni 43 wanaokumbwa na dharura mbali mbali duniani. Flora Nducha na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Flora)

Kwa mara ya kwanza asilimia 25 ya ombi hilo, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kitaelekezwa kwenye elimu kwa watoto walio kwenye majanga ambapo nusu yao ni wale wa Syria walioko nchini mwao nan chi jirani.

UNICEF imesema mamilioni ya watoto wameporwa haki yao ya elimu kutokana mizozo licha ya kwamba elimu ni silaha bora.

Sikander KHAN, ni mkurugenzi wa ofisi ya UNICEF Geneva akihusika na mipango ya dharura.

(Sauti ya Sikander)

“Kama mnavyofahamu mwaka wote wa 2015 na miaka iliyotangulia, imetambuliwa sasa kuwa elimu ni silaha kuu kwenye majanga, sambamba na ulinzi na kudhibiti ghasia na ukiukwaji wa haki. Hayo ni mambo muhimu katika kuepuka kupoteza kizazi.”