Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 500 zasakwa kusaidia wakimbizi CAR na Nigeria

Dola milioni 500 zasakwa kusaidia wakimbizi CAR na Nigeria

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake Jumatatu ya leo wametoa wito kwa nchi wahisani kuchangia zaidi ya dola nusu milioni mwaka huu ili kusaidia maelfu ya watu wanaolazimika kukimbia machafuko Nigeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, pamoja na jamii zinazowapokea na kuwapa malazi na huduma zingine muhimu.

Mikakati miwili ya kusaidia wakimbizi hao iliyowasilishwa kwa wahisani mjini Yaunde Cameroon inajumuisha dola zaidi ya milioni 198 kwa ajili ya wakimbizi wa Nigeria zaidi ya 230,000 na jamii zinazowahifadhi nchini Niger, Chad, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Congo Brazzaville.

Mikakati hiyo miwili itashughulikia mahitaji ya ulinzi, elimu, usalama wa chakula, afya na lishe, maisha yao, malazi, msaada wa msingi, maji, na usafi. Ombi la msaada wa CAR limetolewa na mashirika 25 ikiwemo UNHCR, mashirika mengine ya misaada na mashirika yasiyo ya kiserikali NGO’s, huku ombi la Nigeria likitolewa na mashirika 28.