OCHA imezindua ombi kusaidia wakimbizi Cameroon mwaka 2016

25 Januari 2016

Serikali ya Cameroon, Umoja wa Mataifa na wadau wake wamezindua mkakati wa kushughulikia mahitaji wa wakimbizi nchini Cameroon, na wakati huo huo kutangaza mipango ya kikanda kwa wakimbizi wa Nigeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), kwa mwaka 2016 kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA). John Kibego na Taarifa kamili.

(Taarifa ya Kibego)

Mwito huo wa kibinaadamu wa Cameroon unalenga kuchangisha dola milioni 282, za kuwezesha juhudi za kuhakikisha ulinzi na kutoa msaada kwa watu milioni 1.1 walioathiriwa na mzozo unaoshamiri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, washambuliaji wa kigeni na mashambulio ya kujitolea mhanga nchi Cameroon.

Kwa sababu hizo waNigeria 70,000 wamekimbilia nchini Cameroon huku raia wa Cameroon wapatao 124,000 wakilazimika kukimbia makaazi yao katika eneo la Kaskazini.

Najat Rochdi, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu nchini Cameroon amesema, mpango huo utashughulikia tatizo la njaa na utapiamlo, usalama na kuhakikisha kuwa watu wanafikia huduma zingine za msingi kama afya, elimu, maji na kujisafi.

.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter