Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO yathibitisha mwaka 2015 umevunja rekodi ya joto duniani:

WMO yathibitisha mwaka 2015 umevunja rekodi ya joto duniani:

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limethibitisha kwamba wastani wa joto kimatifa kwa mwaka 2015 umevunja rekodi zote zilizopita kwa kiwango cha nyuzi joto 0.76C iki ni juu ya wastani wa mwaka 1961-1990 .

Kwa mujibu wa WMO kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2015 kiwango cha joto kilikuwa nyuzi joto 1 Selisiasi juu ya kile kilichokuwa kabla ya zama za viwanda.

Shirika hilo linasema miaka 16 iliyopita imekuwa na joto la kupindukia katika rekodi yao yote katika karne hii, huku mwaka 2015 ukiwa na kiwango cha juu zaidi cha joto kuliko rekodi iliyowekwa mwaka 2014 na ikiashirika mfululizo wa muda mrefu wa joto kuanzia 2011-2015 na kufanya miaka hiyo kuwa ya joto zaidi kuwahi kushuhudiwa katika rekodi.

Kiwango cha joto kwa nchi kavu na baharini mwaka 2015 kwa mujibu wa WMO kimeambatana na sababu nyingi za hali ya hewa ya kupindukia ikiwemo mafuriko, mawimbi ya joto ya kupindukia na ukame mkali.