Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa kuahirishwa kwa uchaguzi Haiti.

Ban asikitishwa kuahirishwa kwa uchaguzi Haiti.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-moon ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi mchini Haiti hivi karibuni uchaguzi ambao ulipangwa kufanyika Januari 24.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa Bwana Ban amewataka wadau wote kufanya kazi kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakamilika bila kuchelewa kupitia ridhaa yenye suluhisho litakalowapa fursa watu wa Haiti kutekeleza haki yao ya kuchagua katika uchaguzi wa Rais na wawakilishi waliosalia wa bunge jipya.

Ban amewataka wadau wote wa kisiasa kupinga aina zote za machafuko na vitisho na kujizuia dhidi ya vitendo vovyote ambavyo vyaweza kuvuruga mchakato wa kidemokrasia na utulivu katika nchi.

Katibu Mkuu amenukuliwa akikariri jukumu la Umoja wa Mataifa katika kuendelea kusaidia Haiti kuimarisha demokrasia na utulivu.