Mtazamo wa serikali ya Burundi kuhusu mzozo ni tofauti na wengine: Balozi Samantha
Ujumbe wa Baraza la usalama uliokuwepo Burundi umehitimisha ziara yake na sasa unaelekea Ethiopia kwa ajili ya mazungumzo zaidi kuhusu Burundi na Somalia.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kiwanja cha ndege mji mkuu Bujumbura, mmoja wa wajumbe kwenye baraza hilo, Balozi Samantha Power wa Marekani amesema baada ya mazungumzo yao na pande zote ikiwemo serikali na vikundi vya kiraia na vyama vya kisiasa na kwamba..….
(Sauti ya Balozi Power)
“Mtazamo wangu kwa upande wa serikali ni kwamba hakuna hisia ya udharura au ya fikra ya kuwepo kwa mzozo kama vile ambavyo sisi tumehisi. Tunadhani hali inaweza kudhibitiwa lakini ili hilo lifanikiwe mashauriano lazima yawe shirikishi, mapana na ya haraka zaidi na haiko dhahiri iwapo mchakato unaoongozwa na Uganda unaweza kuzaa matunda.”
Amesema wajumbe wa Baraza walikuwa wazi katika ujumbe wao kwa Rais kutuma ujumbe thabiti kushiriki kwenye mazungumzo na ujumuishe watu walioko ndani na nje ya nchi.
Na kuhusu jeshi la Muungano wa Afrika kwenda Burundi ambalo ujumbe huo ulikwenda ili kushawishi nchi hiyo ikubali, Balozi Samantha amesema hakukuwepo na maendeleo ya kutosha kuhusu suala hilo na alilobaini ni kwamba..
(Sauti Samantha)
“Nchi iko kwenye mzozo na nadhani Baraza la usalama linalazimika kesho kukutana na Muungano wa Afrika kushauriana na marafiki wa Afrika kuhusu hatua zitakazofuata.”