Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoka Abu Dhabi hadi Afrika - matumizi ya nishati mbadala

Kutoka Abu Dhabi hadi Afrika - matumizi ya nishati mbadala

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya nishati mapema wiki hii wamekuwa na mkutano mjini Abu Dhabi, falme za kiarabu kuhusu nishati za baadaye. Huu ni mkutano wa siku tano uliowakutanisha viongozi na wataalamu wa nishati endelevu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu au ajenda 2030 wakati wa maadhimisho ya wiki ya uendelevu ya Abu Dhabi, au Abu Dhabi Sustainable Week.

Huu ni mkutano uliowakutanisha viongozi na wataalamu wa nishati kujadili nishati mbadala ili kusongesha mbele lengo namba saba la SDGs. Lengo hilo ni miongioni mwa malengo mtambuka, kwani licha ya kuwa na mchango mkubwa katika uhifadhi wa mazingira na kusaidia katika kukabili na kuhimili mabadiliko ya tabianchi, kadhalika huisaidia katika biashara, na uchumi kwa ujumla.

Katibu Mkuu Ban Kin-moon akauambia mkutano huo katika ufunguzi kuwa nishati endelevu kwa bei nafuu zitachangia pakubwa katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuokoa maisha ya watu milioni 4.3 wanaofariki kila mwaka kutokana na vyanzo duni vya nishati. Na zaidi ya hayo sekta binafsi iungane na ile ya umma kuhakikisha nishati bora na nafuu zinapatikana. Ban akaongeza..

(SAUTI BAN)

Miongoni mwa washiriki kutoka sekta binafsi katika mkutano huo ni Caesar Mwangi, Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Sunny Money kutoka Kenya ambayo inahusika na usambazaji wa taa zinaotumia nishati ya jua. Katika mahojiano na Assumpta Massoi wa idhaa hii anaeleza jinsi wanavyosambaza taa ndogo zinazotumia nishati ya jua..

(SAUTI MWANGI)

Nchini Burundi nako nishati mbadala inatumika kusaidia wananchi hususan wenye kipato cha chini na hivyo kuleta ahaueni na ukuaji wa kiuchumi. Ramadhani Kibuga amevinjari kuona hali halisi..

(PACKAGE BURUNDI)