Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wanapaswa kutekeleza kwa vitendo dhamira yao ili kufankisha maendeleo Afrika-Kituyi

Viongozi wanapaswa kutekeleza kwa vitendo dhamira yao ili kufankisha maendeleo Afrika-Kituyi

Kwa miongo minne sasa, mkutano wa jukwaa la uchumi limekuwa na lengo la kuimarisha hali kote ulimwenguni kitu ambacho kimesaidia katika programu ya mikutano ya kila mwaka.

Mkutano huo wa kila mwaka wa Davos, Uswisi ni moja ya kiungo muhimu kinachowakutanisha viongozi mbali mbali kwa ajili ya juhudi za pamoja zinazolenga kuimarisha malengo na ajenda ya viwanda duniani.

Wakati huu kunakoshuhudiwa teknolojia mpya zinazobadilisha jamii na hata uchumi viongozi wanahitajika kubadilishana mawazo kwa ajili ya mustakabali wao na kujiandaa na maisha ya baadaye.

Mmoja wa washiriki wa mkutano wa Davos ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, Dkt.Mukhisa Kituyi ambaye katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa hii anazungumzia ujumbe wake kwa mkutano wa Davos. Hapa anaanza kuelezea baadhi ya mazungumzo waliokuwa nayo.