Ban azipongeza Equatorial Guinea na Gabon kwa nia ya kuataka suluhu ya mzozo

Ban azipongeza Equatorial Guinea na Gabon kwa nia ya kuataka suluhu ya mzozo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha hatua ya kufanyika kwa mkutano wa pande tatu wa mawaziri kuhusu mzozo baina ya Jamhuri ya Equatorial Guinea na Gabon, uliofanyika wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York.

Ban amezipongeza pande zote kwa kuonyesha ari ya kisiasa ya kasi mpya katika mchakato wa kukamilisha makubaliano maalum kwa ajili ya kuyawasilishwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Haki.

Katibu Mkuu anabaini mafanikio yaliyopatikana hadi sasa na nia ya pande zote kufanya kila liwezekanalo ili kupata ufumbuzi wa mgogoro huu wa muda mrefu kabla ya mwisho wa mamlaka yake. Amerejelea utayari wake wa kutoa uzaidizi ili kutatua mgogoro huu.