Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Grandi atembelea Za'atari azungumza na wakimbizi wa #Syria

Grandi atembelea Za'atari azungumza na wakimbizi wa #Syria

Zaatari, kambi ya wakimbizi wa Syria nchini Jordan! Mzozo nchini Syria ukiingia mwaka wa Sita nuru bado haiko machoni mwa wakimbizi waliosaka hifadhi hapa. Maisha kambini hayana uhakika wakati huu ambapo usaidizi wa kimataifa nao umetindikiwa. Kamishna mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa Filipo Grandi akatumia fursa ya ziara yake nchini Jordan kuwatembelea wakimbizi hao. Je nini kilijiri? Assumpta Massoi anakupasha zaidi.