Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

DiCaprio aibwatia sekta ya mafuta na gesi kwenye kongamano la uchumi Davos:

DiCaprio aibwatia sekta ya mafuta na gesi kwenye kongamano la uchumi Davos:

Leonardo DiCaprio ameyabwatia makampuni makubwa ya mafuta na gesi duniani kwa kuwa kwa kuwa na tamaa na kuchangia mabadiliko ya tabia nchi, katika hotuba yake kwenye kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos.

Mtayarishaji na muigizaji huyo nyota wa Hollywood ameyasema hayo mbele ya wakuu wa nchi, mawaziri na wakuu wa makampuni akitoa wito wa kuchukua hatua za haraka za kukabili mabadiliko ya tabianchi.

Mcheza filamu huyo amepokea tuzo maalumu kwa sababu ya kazi zake za mazingira na akasema “hatutaweza kumudu kuruhusu tamaa ya makampuni ya gesi, mafuta na makaa yam awe kuamua mustalhbali wa ubinadamu.”

DiCaprio, anayetarajiwa kushinda tuzo ya Accademy kwa ajili ya filamu yake mpya The Revenant, ameongeza kuwa imetosha, na dunia inalitambua hilo, historia itabebesha lawama za zahma hii kwa makampuni hayo.

Nyota huyo wa filamu pia ameaihidi donge nono la dola milioni 15 kupitia mfuko wake wa Leonardo DiCaprio Foundation ili kusaidia miradi ya kulinda mazingira.