Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa jopo la UM kuhusu afya ya mama na mtoto

Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa jopo la UM kuhusu afya ya mama na mtoto

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza wajumbe wa kwanza wa jopo la ushauri la ngazi ya juu kuhusu afya ya mama na mtoto  #Everywomaneverychild.

Jopo hilo la watu  12 litakuwa na wenyeviti wanne akiwemo Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete, na Waziri Mkuu wa Ethiopita Hailemariam Desalegn. Wengine ni Rais wa Chile Michelle Bachelet na Rais wa zamani wa Finland Tarja Halonen.

Ban amesema jopo hilo litamshauri jinsi ya kusaidia kuonyesha uongozi katika masuala ya afya ya wanawake, watoto na vijana barubaru wakati huu ambapo dunia inahama kutoka malengo ya maendeleo ya milenia kuanza kutekeleza malengo endelevu, SDGs.

Wenyeviti hao watafanya kazi wawili wawili kwa kipindi cha mwaka mmoja mmoja wakipokezana na jopo litakuwa na linakutana mara mbili kwa mwaka.

Mkakati wa kimataifa wa afya ya wanawake, watoto na barubaru pamoja na kutoa mwelekeo kupitia afya ya mama na mtoto ili kumaliza vifo vya makundi hayo vitokanavyo na magonjwa yote yanayozuilika ifikapo mwaka 2030, pia unalenga kuhakikisha ustawi wao katika utekelezaji wa SDGs.