Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirikiano wa kimataifa unafanikiwa kukiwa na mipango kabambe:Ban

Ushirikiano wa kimataifa unafanikiwa kukiwa na mipango kabambe:Ban

Umoja wa mataifa umedhihirisha kwamba palipo na mipango kabambe basi ushirikiano wa kimataifa unafanikiwa, hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipozungumza leo kwenye kikao cha mshikamano wa kimataifa Global Compact kandoni mwa mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya uchumi mjini Davos Uswisi.

Ban amesema ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu na makubaliano ya tabia nchi ya Paris ni mitazamo ya kidunia ambayo inaweza kubadili historia ya dunia endapo ahadi zilizotolewa zitatimizwa.

(SAUTI YA BAN 1)

“Tunahitaji uongozi wenu imara, ushiriki wenu na kujizatiti kwenyu. Nyie ndio wenyewa maderava muhimu sana katika kulifanikisha hili."

Ameongeza kuwa wakati huo huo biashara zinaweza kutoa suluhu muhimu na rasilimali ambazo zitaiweka dunia yetu katika njia endelevu. Amesema ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu na na makubaliano ya Paris ni hatua ya mabadiliko na kwamba

(SAUTI BAN 2)

“Malengo ya maendeleo endelevu kwanza ni ya dunia nzima, yanayoingiliana ni malengo binafsi, hakuna kinachoweza kugawanya au kuyatenga malengo hayo 17, kila kitu lazima kiende pamoja na ukiwa na mtazamo huo nina uhakika tutafanikiwa”