Skip to main content

Baraza la Usalama lamulika Cote d’Ivoire

Baraza la Usalama lamulika Cote d’Ivoire

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu hali nchini Cote d’Ivoire ambapo limepatiwa ripoti kuhusu operesheni za Umoja huo kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Taarifa zaidi na  Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Nats…

Kikaoni Baraza la usalama, Rais wa kikao Balozi.. akitangaza kupitishwa kwa kauli moja kwa azimio namba S/2016/47 kuhusu Cote d’Ivoire.

Nats…

Azimio pamoja na mambo mengine linapunguza idadi ya askari kutoka 5,437 hadi 4,000 ifikapo Machi 2016.

Wajumbe pia walipatiwa ripoti ya Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu  utendaji wa ujumeb wa Umoja huo nchini Cote d’Ivore, UNOCI.

Ripoti hiyo pamoja na kupongeza uchaguzi wa amani nchini  humo inaeleza azma ya Katibu Mkuu ya kutuma ujumbe Cote d’Ivoire ambao kwa mashauriano ya serikali na wadau wote husika utahakikisha ifikapo Machi 31 mwaka huu kuna mapendekezo ya UNOCI kuhitimisha shughuli zake nchini humo.

Kwa mantiki hiyo azimio limemtaka Katibu Mkuu awe amelipatia Baraza mapendekezo ya kuondoka kwa UNOCI lakini kwa kuzingatia hali ya usalama nchini humo.