Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila ya ufadhili katika sekta ya kilimo Syria itaangamia zaidi:FAO

Bila ya ufadhili katika sekta ya kilimo Syria itaangamia zaidi:FAO

Wakati mapigano yanapamba moto Syria kwa mwaka wa sita sasa, sekta ya kilimo nayo inaangamia pole pole na kuwatumbukiza mamilioni ya watu katika njaa, na kusababisha kasi ya upungufu wa tija na kupanda kwa bei ya chakula, limesema Shirika la Chakula na Kilimo FAO.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

FAO leo imetoa wito kwa serikali kupiga jeki mfuko wa fedha utakaowasaidia wakulima nchini humo kuendeleza shughuli za kilimo ili hali isiwe mbaya zaidi. Wito huu unakuja kabla ya Mkutano wa Kimataifa wa Ufadhili utakaofanyika jijini London tarehe 4 Februari. Mkutano huo umeitishwa na Uingereza, Ujerumani, Norway, Kuwait pamoja na Umoja wa Mataifa kuhamasisha msaada wa kibinaadamu kwa Syria.

Dominuque Burgeon ni Mkuu wa Kitengo cha Dharura cha FAO, na hapa anaelezea umuhimu wa ufadhili katika sekta ya kilimo..

" kuwekeza katika kilimo hakutasaidia tu wakulima kubaki katika mashamba yao bali pia kutapunguza mzigo mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa, wakati huu ambapo gharama zinazoletwa na mgogoro wa Syria zimekuwa ni mzigo mkubwa usioweza kubebeka"