Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunafuatilia kirusi cha Zika- Tanzania

Tunafuatilia kirusi cha Zika- Tanzania

Serikali ya Tanzania imesema inafuatailia kwa karibu taarifa za za uwepo wa kirusi aina ya Zika ambacho kimeelezwa na shirika la afya ulimwenguni WHO kupatikana kwenye mataifa 18 duniani ikiwemo Uganda.

Kirusi hicho kinachoenezwa na mbu aina  ya Aedes kinadaiwa kuwa na uhusiano na watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo na mpaka sasa WHO inaendelea na utafiti kubaini iwapo ni kweli au la.

Katika mahojianio ana idhaa hii Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini humo Dkt. Janeth Mghamba ametaja hatua zinazochukuliwa na Tanzania.

(SAUTI DK JANETH)

WHO imesema kirusi hicho kimeripotiwa katika mataifa ya Amerika, Afrika na Pasifiki Magharibi na ndicho kinachosababisha ugonjwa wa Dengeu, Chikungunya na homa ya manjano.