Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufaransa yatakiwa kulinda uhuru wa watu inapokabiliana na ugaidi

Ufaransa yatakiwa kulinda uhuru wa watu inapokabiliana na ugaidi

Hali ya sasa ya dharura nchini Ufaransa na sheria ya ufuatiliaji wa mawasiliano ya elektroniki unaweka vikwazo vya kupita kiasi na visiyvo na uwiano dhidi ya uhuru wa kimsingi wa watu , limeonya leo kundi la Umoja wa Mataifa la wataalam wa haki za binadamu .

Katika orodha ya vitu vinavyowatia hofu walivyoileza serikali ya Ufaransa wataaalamu hao huru, wamesisitiza ukosefu wa uwazi na usahihi wa masharti kadhaa ya hali ya sheria ya dharura na ufuatiliaji, kuhusiana na aina na upeo wa vikwazo kwa utekelezaji wa haki ya uhuru wa kujieleza, uhuru wa mikutano ya amani na kuijiunga na chama na haki ya faragha.

Wamesema wakati Ufaransa inajadili kuimarisha hatua za vita dhidi ya ugaidi na kufikia kufanya mabadiliko ya mfumo wa kukabiliana na uhalifu wametoa wito kwa serikali , kurekebisha masharti na uwezekano wa mageuzi yaliyopitishwa kufikia lengo hilo, ili kuhakikisha kuwa yanazingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu.

Ili kuhakikisha utawala wa sheria na taratibu za kuzuia hatua za kiholela, wataalam wamependekeza kupitishwa kwahatua za awali za udhibiti wa mahakama katika  kupambana na ugaidi.