Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi yakaribisha wajumbe wa Baraza la usalama

Burundi yakaribisha wajumbe wa Baraza la usalama

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatarajia kufanya ziara ya siku mbili nchini Burundi katika juhudi za kukwamua mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Serikali ya Burundi imekaribisha ziara hiyo kwa kusema ni fursa ya kushuhudia hali halisi inayojiri  Burundi.

Kutoka Bujumbura, Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga anaarifu zaidi.

(TAARIFA YA KIBUGA)