Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa haki za binadamu wakaribisha kuachiliwa kwa raia wa Marekani Iran

Wataalamu wa haki za binadamu wakaribisha kuachiliwa kwa raia wa Marekani Iran

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa leo wamekaribisha  hatua ya serikali ya Iran ya kuwaachilia huru raia wanne wa Marekani wenye asili ya Iran na kuitolea wito serikali ya Tehran kufungua mlango wa kuachiliwa mahabusu wote wanaoshikiliwa kinyume cha sheria  katika magereza ya nchi hiyo.

Mwishoni mwa juma maafisa wa serikali ya Iran walitangaza kwamba raia wane wa Marekani wenye asili ya Iran akiwemo ripota wa gazeti la Washington Post Jason Rezaian, Kasisi wa Kikristo Saeed Abedini na Amir Hekmati wameachiliwa kutoka magerezani kutokana na hatua ya kubadilishana wafungwa na Marekani.

Bwana Rezaian na Bwana  Abedini walishitakiwa kwa upelelezi na makossa mengine yanayohusiana na usalama wa taifa na uhalifu katika katika kesi ambazo hazikuwa na viwango  vya kimataifa.

Na kwa mwaka mmoja na nusu uliopita, Bw Rezaian kushikiliwa kwake kizuini kinyume cha sharia kumedhihirisha jinsi serikali ya Iran serikali inavyokandamiza uhuru wa kujieleza na wa waandishi wa habari nchini humo, amesema David Kaye mwandishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa ripoti kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza.