Skip to main content

UNMISS yaweka kambi ya matibabu kwa wakazi wa Malakal na Upper Nile

UNMISS yaweka kambi ya matibabu kwa wakazi wa Malakal na Upper Nile

Walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS wameendesha huduma ya bure ya kambi ya matibabu waliyoiweka maalumu kwa ajili ya jamii za Malakal, Upper Nile.

Walinda Amani hao kutoka jeshi la wanamaji la Bangladeshi wamejitolea kutoa huduma za msingi za matibabu kwa wakazi kwenye kituo kipya kwenye ukingo wa Magharibi wa mto Nile.

Jumla ya watu 229 wakiwemo wanawake na watoto wamepatiwa matibabu. Kliniki hiyo ya siku moja imezilenga jamii hizo za ukingo wa magharibi ambazo hazina fursa na kambi ya Umoja wa Mataifa iliyoko upande wa pili wa mto. Kamanda wa walinda Amani hao anafafanua...

Timu hiyo imejumuisha Daktari mmmoja na wauguzi wanawane.