Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tisho la El nino laongezeka msimu wa kupanda ukikaribia Kusini mwa Afrika:

Tisho la El nino laongezeka msimu wa kupanda ukikaribia Kusini mwa Afrika:

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linazidi kuhofia usalama wa chakula Kusini mwa Afrika ambako watu takribani milioni 14 wanakabiliwa na njaa kufuatia ukame uliosababisha mavuno hafifu mwaka jana. Priscilla Lecomte na taarifa kamili

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Kwa mujibu wa WFP majira ya El Nino ambayo yanachangia hali kuwa mbaya Zaidi ukanda mzima tayari yameathiri mazao ya mwaka huu.

Wakati huu kukiwa na mvua kidogo au hakuna kabisa katika maeneo mengi huku fursa ya kupanda ikitoweka hraka au kumalizika katika baadhi ya nchi hali inatia hofu.

WFP inasema idadi ya watu wasio na chakula inaweza kuongezeka haraka katika miezi ijayo kwenye msimu wa palizi kabla ya muda wa mavuno hapo mwezi April ambapo akiba ya chakula na fedha hutoweka. Imeongeza kuwa na waathirika wakubwa katika hali hii ni wakulima wadogowadogo.