Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za kukabiliana na ugaidi kutishia fedha zinazotumwa nyumbani na Wasomali wa ughaibuni

Hatua za kukabiliana na ugaidi kutishia fedha zinazotumwa nyumbani na Wasomali wa ughaibuni

Utumwaji wa fedha nyumbani kutoka kwa Wasomali waishio ughaibuni kunatishiwa na hatua za lazima za kukabiliana na ugaidi lakini ambazo hazikufikiriwa vyema. Amina Hassan na taarifa kamili

(TAARIFA YA AMINA HASSAN)

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba hatari za hatua hizo zinaathiri pakubwa haki za binadamu za watu wa Somalia na wamezitaka serikali za Marekani, Uingereza, Australia na Somalia kuhakikisha kwamba zoezi hilo la kuingia kwa fedha linaendelea.

Kumekuwa na taarifa nyingi hivi karibuni za Wasomali walioko ughaibuni kupata shida ya kutuma fedha nyumbanikwa sababu bank za biashara katika nchi wanakotuma zinafunga akaunti za waendeshaji za kuhamisha fedha Somalia za waendeshaji katika kukabiliana na masharti magumu na kanuni za ndani na nje za kupambana na fedha haramu na ufadhili wa ugaidi. Bahame Nyanduga ni mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Somalia.

(SAUTI YA NYANDUGA)