Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani shambulio la kigaidi mjini Ouagadougou, Burkina Faso

Ban alaani shambulio la kigaidi mjini Ouagadougou, Burkina Faso

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi lililotokea jana Ijumaa mjini Ouagadougou, Burkina Faso, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20 na kujeruhi wengine wengi.

Ban ambaye ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu wa waarithika, watu wa Burkina Faso na serikali , pia amewatakia nafuu ya haraka majeruhi na kurejea kusisitiza kuwa Umoja wa mataifa unashikamana na serikali ya Burkina Faso na ukanda mzima na upo tayari kusaidia katika vita vyake dhidi ya ugaidi.

Ametoa wito kwa uongozi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha inawafikisha kwenye mkono wa sheria haraka waliohusika na shambulio hilo.