Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya raia wa Msumbiji wanaowasili Malawi inaongezeka :UNHCR

Idadi ya raia wa Msumbiji wanaowasili Malawi inaongezeka :UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema idadi ya watu wanaokimbia Msumbiji na kutafuta hifadhi nchini Malawi imeongezeka sana katika wiki chache zilizopita.

Katika kijiji cha Kapise, wilaya ya Mwanza kilometa chache kutoka mji mkuu Lilongwe , timu ya UNHCR imeorodhesha watu  1,297 waliowasili huku theluthi mbili wakiwa wanawake na watoto na watu wengine Zaidi ya 900 wanasubiri kusajiliwa.

Watu wengine 400 wamearifiwa kuwasili katika vijiji 16 vilivyoko kwenye wilaya ya Chikwawa. Flora Nducha amezungumza na Moses Okumu  afisa wa UNHCR Malawi ambaye anaanza kueleza lini watu hao walianza kuingia Malawi.

(MAHOJIANO NA MOSES OKUMU)