Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maadhimisho ya muongo wa watu wenye asili ya afrika

Maadhimisho ya muongo wa watu wenye asili ya afrika

Kwa zaidi ya miaka mia 400, biashara ya utumwa imekuwa janga lililoikumba Afrika, ikikadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni 15, wanaume, watoto na wanawake wamekuwa wahanga wa biashara hii kupitia bahari ya Atlantiki.

Hadi leo, Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba watu wapatao milioni 200 wenye asili ya Afrika wanaishi Marekani na kwenye bara la Amerika na Karibia.

Wengi wao bado hukumbwa na unyanyapaa na ubaguzi, wakikosa fursa sawa za kielimu, kisiasa na kiuchumi.

Mwaka 2014, Umoja wa Mataifa umeamua kuadhimisha muongo wa watu wenye asili ya Afrika ili kutambua historia hii na matatizo yanayokabili watu hawa, kupambana na ubaguzi na kuchukua hatua ili kuleta maendeleo na usawa zaidi kwa ajili yao.

Katika mwendelezo wa maadhimisho  hayo, Wiki hii, maonyesho maalum yamezinduliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhusu muongo huo, Priscilla Lecomte amehudhuria maonyesho hayo.