Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa na Zimbabwe kuanzisha mpango wa kukabiliana na El-nino

Umoja wa Mataifa na Zimbabwe kuanzisha mpango wa kukabiliana na El-nino

Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe yamekutana leo mjini Harare kujadili athari zilizosababishwa na El-Nino nchini humo na kutayarisha mpango wa dharura ili kukabiliana na tatizo hilo.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo imesema kwamba huenda hali ya ukame inaweza kuwa mbaya zaidi mwaka 2016 ikilinganishwa na mwaka 2015, watu milioni 1.5 wakitarajiwa kukumbwa na uhaba wa chakula nchini Zimbabwe kwa kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka huu.

Umoja wa MAtaifa umetoa wito kwa ufadhili, ukieleza kwamba dola milioni 59 tu zilikuwa zimefadhiliwa kutoka kwa mpango wa kitaifa wa dola milioni 132 uliotangazwa mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Miongoni mwa harakati zinazohitaji usaidizi ni ukarabati wa miundombinu za umwagiliaji nchini humo.

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba watu wapatao milioni 30 wamekumbwa na njaa kwenye ukanda wa Afrika Kusini.