Skip to main content

AMISOM yashambuliwa na Al-Shabaab Somalia

AMISOM yashambuliwa na Al-Shabaab Somalia

Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika nchini Somalia, Balozi Francisco Madeira, amelaani vikali mashambulizi yaliyotokea leo alfajiri kwenye kituo cha ujumbe wa Muungano huo nchini Somalia, AMISOM huko El Adde, kwenye eneo la Gedo nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na AMISOM shambulio hilo la kigaidi limefanywa na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab.

AMISOM imesema shambulio hilo limesababisha vifo na majeraha lakini bado taarifa zinapaswa kuthibitishwa kuhusu idadi.

Imeeleza zaidi ikisema kwamba askari wa AMISOM walipambana na waasi wa Al-Shabaab na kuwarudisha nyuma na Balozi Madeira amewapongeza kwa wepesi na ushujaa wao.

Aidha Balozi Madeira ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwataia nafuu waliojeruhiwa.