Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atangaza mpango dhidi ya misimamo mikali

Ban atangaza mpango dhidi ya misimamo mikali

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza mpango wake wa kukabiliana na ghasia zinazochagizwa na misimamo mikali akisema ni muhimu kwa kuwa vitendo hivyo ni shambulizi la moja kwa moja dhidi ya katiba inayounda chombo hicho.

Akitangaza mbele ya Baraza Kuu, Ban amesema mpango wake wa utekelezaji wenye mapendekezo 70 yanayojikita kwenye misingi mikuu mitano unalennga kudhibiti vichochezi vya ghasia hizo ambazo zinaweza kusababisha ugaidi. Misingi hiyo ni mosi kuzuia akisema..

(Sauti ya Ban)

“Hakuna njia moja inayosababisha bali twafahamu misimamo mikali inashamiri pindi haki za binadamu zinapokiukwa, ushiriki wa kisiasa kubinywa, matarajio ya watu hasa vijana kupuuzwa na ifahamike kukosa matumaini ni kupoteza maisha.”

Pili ni uongozi thabiti unaozingatia kanuni, tatu kuzingatia haki za binadamu, Nne sera za uongozi bora na maendeleo endelevu kwa kuzingatia eneo husika na tano ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika kusaidia nchi wanachama kukabili vichochezi vya misimamo mikali.

Ban amesema baadhi ya nchi wanachama tayari zimeahidi kuridhia mpango huo kuwa halisia na hivyo ni anasubiri kwa hamu mkutano wa mwezi Aprili uliondaliwa na serikali ya Uswisi kuhusu mpango huo dhidi ya misiamo mikali.