FAO kukabiliana na ukame Ethiopia
Nchini Ethiopia, Shrika la chakula na kilimo FAO linasema ukame uliokumba nchi hiyo kwa takribani miongo mitatu kutokana na ukame uliosababishwa na mvua za El-Nino umesababisha watu zaidi ya milioni 10 kukumbwa na njaa , huku mifugo ikiwa imekufa kwa wingi na mazao kuharibika. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.
(Taarifa ya Priscilla)
FAO ambayo imezindua leo mpango wa dharura wa dola milioni 50 kwa ajili ya kukabiliana na mzozo huo, imeeleza kwamba mazao imepungua kwa asilimia 50 hado 90 kwenye baadhi ya maeneo ya nchi, na malaki ya mifugo imekufa. Hali inatarajiwa kuendelea kuzorota kutokana na ukosefu wa maji hadi mwanzo wa msimu wa mvua mwezi Machi, huku msimu wa kupanda mbegu ukikuwa unatakiwa kuanza mwezi huu.
Msaada wa FAO unalenga wakulima takriban milioni 1.8 kupitia miradi mbali mbali ikiwemo usambazaji wa mbegu na vyakula kwa mifugo pamoja na utekelezaji wa miradi ya umwagiliaji.
FAO imeanzisha mipango ya dharura kwa ajili ya kupambana na madhara ya El-Nino kwenye nchi 20 zilizoathirika zaidi, kote duniani.