Mfanyakazi wa UNEP ajeruhiwa katika mashambulio ya kigaidi Jakarta

Mfanyakazi wa UNEP ajeruhiwa katika mashambulio ya kigaidi Jakarta

Mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira (UNEP) amejeruhiwa vibaya katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika leo Alhamisi kwenye maeneo ya jirani na ofisi za Umoja wa Mataifa katikati ya mji wa Jakarta. Assumpta Massoi na Taarifa kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Mfanyakazi huyo raia wa Uholanzi ni mtaalamu wa masuala ya misitu na usimamizi wa mazingira alikuwa Jakarta kama sehemu ya timu ya Umoja wa Mataifa inayotoa msaada kwa serikali ya Indonesia wa kukabiliana na moto usababishwao na mboji.

Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Achim Steiner amesema shirika hilo linalaani vikali vitendo hivyo vya kigaidi na kwamba fikra na sala zao ziko pamoja na familia za waathirika ikiwemo ya mfanyakazi mwenzao pamoja na watu na serikali ya Indonesia. Mfanyakazi huyo ameoa na ana watoto wane.