Skip to main content

Shambulio Pakistani laua watu 15, Ban alaani

Shambulio Pakistani laua watu 15, Ban alaani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio lililotokea leo kwenye kituo cha utoaji wa chanjo dhidi ya Polio nchini Pakistani.

Shambulio hilo katika mji wa Quetta limesababisha vifo vya watu wapatao 15 huku wengine 25 wamejeruhiwa.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Ban akituma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na serikali ya Pakistani huku akiwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Halikadhalika amesisitiza tena kuwa hakuna jambo lolote linalohalalisha ugaidi.

Ameisihi serikali ya Pakistani kuchukua hatua zote muhimu kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa shambulio hilo.