Kushikamana na Kutegemeana ni kanuni za Ajenda ya 2030 : Eliasson

13 Januari 2016

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ni ajenda ya karne ya 21 inayounganisha nchi zote kote duniani.

Akihutubia kikao kilichofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekeni kuhusu maadili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, amesema kanuni za malengo hayo ni mshikamano, kutegemeana na umoja wa kimataifa.

Amesema jambo la msingi ni kwamba malengo hayo yanalenga zaidi watu wanaoteseka zaidi ili kuhakikisha hakuna mtu mmoja anayeachwa nyuma akisema.

(Sauti ya Bwana Eliasson)

“Tunapaswa kuhakikisha kwamba SDGS zinageuka ukweli kwa mamilioni ya watu ambao wanategemea na kustahili mabadiliko mazuri. Hii huenda ikawa changamoto yetu kubwa zaidi ya kimaadili : kuyafanya maazimio yetu yageuke ukweli kwa watu waliopo nje, watu tunaowahudumia.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter