Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kimataifa wa elimu kama chachu ya SDG’s wamalizika India:

Mkutano wa kimataifa wa elimu kama chachu ya SDG’s wamalizika India:

Mkutano wa kimataifa wa siku tatu wa kutambua elimu kama mwezeshaji muhimu wa utambuzi mpana wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s unamalizika leo mjini Ahmedabad nchini India.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ni muhimu kwa jamii kuangalia kila lengo la SGD na kubaini jinsi gani elimu inaweza kusaidia kulifikia lengo hilo.

Lengo kuu la mkutano huo uliowaleta pamoja wataalamu wa kimataifa 500 katika nyanja ya elimu ni kubadilishana mawazo kuhusu jukumu la elimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Irina Bokova ni mkurugenzi mkuu wa UNESCO.

(SAUTI YA BOKOVA)

"Ni lazima elimu iwe msingi wetu ili kuleta maadili mapya na tabia mpya kwa karne zijazo. Huu ndio umuhimu wa programu ya kuchagiza hatua kote ulimwenguni ya UNESCO kwa ajili ya elimu kwa maendeleo endelevu."