Skip to main content

UM kutathimini njia za kuwajumuisha katika jami walioachiliwa na Boko Haram:

UM kutathimini njia za kuwajumuisha katika jami walioachiliwa na Boko Haram:

Watalaamu watatu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa watazuru Nigeria kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwezi huu ili kutathimini njia za kusaidia kuwajumuisha katika jamii wanawake na watoto waliotoroka au kuokolewa kutoka kwenye mikono ya kundi la Boko Haram. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA )

Kwa mujibu wa wataalamu hao Maud de Boer-Buquicchio, mwakilishi maalumu kuhusu uuzaji wa watoto, Urmila Boola,mwakilishi kuhusu utumwa na Dainus Pûras mwakilishi kuhusu haki ya afya, ni kwamba hatua zote zitakazochukuliwa au kupangwa kuchukuliwa kuhakikisha haki ya huduma, tiba na kuwaunganisha na jamii wanawake hawa na watoto zinapaswa kuzingatia kanuni na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

Wakati wa ziara yao hiyo ya siku tano wataalamu hao watakusanya taarifa kuhusu mitadi mbalimbali iliyopitishwa na serikali, wadau wa kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kuwasaidia wanawake hawa na watoto kukabiliana na mateso makubwa, majeraha, unyanyapaa na uwezekano wa kurejea katika hali ya kawaida.

Pia wataalamu hao walioalikwa na serikali ya Nigeria watakutana na wawakilishi wa wizara mbalimbali, asasi za kijamii na mashirika husika ya Umoja wa Mataifa.