Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM alaani mashambulizi ya bomu misikitini Iraq

Mwakilishi wa UM alaani mashambulizi ya bomu misikitini Iraq

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Iraq Ján Kubiš, amelaani mashambulizi ya mabomu dhidi ya misikiti sita kwenye eneo la Muqdadiya jimbo la Diyala nchini Iraq.

Amesema kwa mara nyingine maeneo ya ibada yanashambuliwa, na waliotekeleza wanataka kuchochea ghasia za kidini wakiwa na hamasa ya kutaka kuirejesha nchi katika siku za giza za machafuko ya kidini.

Bwana Kubis ametoa wito wa pande zote kujizuia kutoingizwa kwenye mzunguko wa chuki kutokana na vitendo hivi vya kinyama ambavyo vina lengo la kugombanisha miongoni mwa makundi mbalimbali kwenye jamii ya Wairaq.

Kubiš pia amelaani mashambulio mengine kwenye eneo la maduka mjini Baghdad na bomu lililokuwa limetegwa kwenye gari ambalo limekatili maisha