Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani vikali shambulio la bomu Uturuki lililoua 10

Umoja wa Mataifa walaani vikali shambulio la bomu Uturuki lililoua 10

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amealaani shambulio la kigaidi alilooliita  la kupuuzwa huko Sultanahmet nchini Uturuki lililosababisha vifo vya watu 10 na kujerhi takribani 15.

Taarifa ya Katibu Mkuu kupitia ofisi ya msemaji wake inasema kuwa Bwana Ban anatarajia kuwa  watakelezaji wa shambulio hilo watafikishwa katika vyombo vya sheria huku akituma rambirambi zake kwa serikali na watu wake pamoja na serikali ya Ujerumani na raia wengine wa kigeni waliuohusishwa na bomu hilo. Amewatakia majeruhi uponyaji wa haraka.

Katika hatua nyingine mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika  muungano wa ustaarabu Nassir Abdulaziz Al-Nasser,amelaani vikali shambulio la bomu ambalo limeua watu kumi na kujeruhi wengine 15 katika wilaya ya  Sultanahmet mjini Istanbul Uturuki leo.

Taarifa ya msemaji wa kiongozi huyo  inamkariri Bwana Al-Nasser akielezea kuhuzunishwa na shambulio hilo ambalo limelenga watu wasio na hatia na kukariri kuwa matukio kama hayo ni tishio kwa amani na usalama na kinyume na maadili ya stahamala.

Amesema kuwa shambulio hilo pia ni kinyume na maadili ya majadiliano ya amani na heshima kwa pande zote ambao ni msingi wa katika kuasisi lengo la Muungano wa Umoja wa Mataifa wa ustaarabu ambao serikali ya Uturuki ni mfadhili mwenza.

Bwana Al-Nasser ameitaka jumuiya ya kimataifa kusalia wamoja  na msimamo wa kuwa kinyume na ugaidi na kukabiliana na aina zote za ugaidi wakati huu ambapo tukio hili la kutisha likiripotiwa. Kadhalika ametuma salamu za rambirambi kwa waathiriwa, familia na serikali na watu wa Uturuki na kusema kuwa muungano anaouongoza unaiombea serikali na watu wake.