Skip to main content

Nepal: Ujumbe wa akiolojia wa UNESCO kuanzisha mbinu kukabili athari baada ya maafa

Nepal: Ujumbe wa akiolojia wa UNESCO kuanzisha mbinu kukabili athari baada ya maafa

Tetemeko la ardhi la 2015 nchini Nepal halikuwa tu zahma kubwa kwa binadamu bali pia lilisababisha athari kubwa kwa utamaduni nchini humo likiharibu urithi wa kipekee wa nchi hiyo.

Urithi huo ambao una nafasi kubwa katika maisha ya watu na chanzo kikuu cha pato la utalii utajengwa upya mwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO.

Ujumbe maalumu wa masuala mbalimbali ya ukozi wa akiolojia unaodhaminiwa na UNESCO uliwasili Kathmandu kwenye maeneo ya urithi wa dunia kati ya Oktoba 5 na Novemba 22 mwaka jana kutathimini hali kabla ya ujenzi.

Ujumbe huo umeelezea jukumu la akiolojia katika kutoa muongozo wa kukabiliana na athari , ujenzi mpya na ukarabati wa urithi ulioharibika. Maeneo waliyoyatilia mkazo ni Bhaktapur na Patan yaliyopo Durbar square mjini Kathmandu.