Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji zaidi ya 18,000 wamevuka kusaka hifadhi Ulaya kwa siku 11:IOM

Wahamiaji zaidi ya 18,000 wamevuka kusaka hifadhi Ulaya kwa siku 11:IOM

Shirika la kimataifa la uhamaiaji IOM linasema zaidi ya wahamaiji 1,700 huvuka kila siku kwa kutumia bahari kusaka hifadhi barani Ulaya,  takwimu hizi zikiwa ni za siku 11 za mwanzo wa mwaka 2016. Idadi hii imefanya wahamiaji kufikia kiasi cha zaidi ya elfu kumi na nane hadi sasa.

Mmoja wa wafanyakazi wa IOM mjini Roma Italia Flavio Di Giacomono, amesema jumatatu mamalaka nchinihumo imegundua miili ya wanawake inayosadikika ilitoswa baharini na maharamia pamoja na wahamiaji wengine 37 wa Somalia ambao walitoka salama katika chombo hicho.

IOM inasema kuwa wahamiaji weingine wanane hawajulikani waliko huku pia wengine 220 wakiokolewa baharini wakiwa njiani kuelekea Italia katika kipindi hicho cha siku 11.

Kwa mujibu wa IOM vifo vya zaidi ya wahamiaji na wakimbizi 3,000 mwaka jana 2015 katika bahari ya Mediterranean vimewekwa rikodi ya kipekee.