Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubelgiji imechangia Euro milioni 2.45 kusaidia wakimbizi wa Palestina:UNRWA

Ubelgiji imechangia Euro milioni 2.45 kusaidia wakimbizi wa Palestina:UNRWA

Serikali ya Ubeligiji imetoa mchango wa Euro milioni 2.45 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA ikiunga mkono shughuli za shirika hilo katika kutoa huduma kwa wakimbizi kwenye maeneo yanayokaliwa ya Wapalestina.

Mchango huo utagawanywa baina ya mradi wa UNRWA wa kusaidia makazi kwenye Ukanda wa Gaza na mpango wa kusaidia programu ya afya ya akili, inayowalenga wasiojiweza kwenye jamii ya Mabedouin Ukingo wa Magharibi.

Machafuko ya mwaka 2014 Gaza yaliathiri makazi zaidi ya 140,00 ya wakimbizi wa Palestina na kusambaratisha kabisa nyumba zaidi ya 9000.

Mchango huo wa Ubelgiji utawasaidia Wapalestina kukarabati na kujenga upya nyumba zao hasa wakati huu ambapo ukosefu wa fedha umewaacha maelfu kushindwa kukarabati nyumba zao.

Ufalme wa Ubelgiji ni mshirika mkubwa wa UNRWA tangu mwaka 1953 na umeshachangia zaidi ya dola milioni 90 kwa shirika hilo tangu mwaka 2007.