Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu mpya wa UNAMID Martin Uhomoibhi awasili Dafur:

Mkuu mpya wa UNAMID Martin Uhomoibhi awasili Dafur:

Mkuu mpya wa vikosi vya pamoja vya vya kulinda Amani Dafur vya Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID amewasili El Fashar, Kaskazini mwa Dafur Jumatatu kuanza rasmi majukumu yake. Amina Hassan na taarifa kamili.

(TAARIFA TA AMINA)

ACTUALITY: FANFARE, PARADE….

Hivyo ndivyo alivyopokelewa Dr. Martin Uhomoibhi (Pron:Umwobi) raia wa Nigeria anayechukua nafasi ya Abidoun Bashua aliyekuwa kaimu kwa muda. Bwana Umwobi ambaye pia amepata fursa ya kukutana na walinda Amani wa UNAMID, baadhi ya wananchi wa Dafur na viongozi wa serikali, amesema lengo ni kuhakikisha wanasaidia pande husika kufikia suluhu ya Amani ya kudumu.

(CLIP UHOMOIBHI)

“Niko hapa kuendeleza kazi nzuri na kuhakisha kwamba amani ambayo watu wetu wazuri hapa wanastahili inarejeshwa. Pia kurejesha nia njema ya Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika na nia yangu binafsi pamoja na watenda kazi pamoja name”.

Dr. Uhomoibhi , mwanadiplomasia wa muda mrefu na aliyewahi kuwa rais wa baraza la haki za binadamu kama anavyoeleza Jumbe Omari Jumbe mkuu wa Radio UNAMID pia ana changamoto mbele yake.

(CLIP JUMBE OMARI JUMBE)