Skip to main content

UM na Ulaya waitaka Marekani ifunge gereza la Guantánamo

UM na Ulaya waitaka Marekani ifunge gereza la Guantánamo

Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na Ulaya wameitaka Marekani ikomeshe ukwepaji sheria katika usimamizi wa haki za binadamu na ifunge gereza la Guantanamo.Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Wataalamu hao kupitia barua yao ya wazi wamesema Marekani kwa kutumia gereza hilo lililoanza kushikiliwa wafungwa miaka 14 iliyopita, imekuwa ikikiuka haki za binadamu na hivyo ichukue hatua kwanza kujisafisha yenyewe.

Wamesema usalama wa muda mrefu unaweza kupata hakikisho kwanza kwa kufunga kituo hicho ambacho kimekuwa cha madhila katika utekelezaji wa hatua dhidi ya ugaidi baada ya shambulio la mwezi Septemba mwaka 2001.

Wamerejelea kuwa zaidi ya watu Mia Moja wanashikiliwa kwenye gereza hilo bila kesi zao kusikilizwa licha ya agizo la Rais Barack Obama wa Marekani la mwaka 2009 la kutaka waachiliwe huru au wahamishiwe ili gereza hilo lifungwe.

Miongoni mwa wataalamu hao ni Ben Emmerson anayehusika na uhuru wa mahakam na Mónica Pinto Mwenyekiti wa jopo la kikundi cha Umoja wa Mataifa kuhusu ushikiliwaji holela wa watuhumiwa.