Skip to main content

Uchumi Afrika kuendelea kukua 2016 , lakini changamoto bado zipo:

Uchumi Afrika kuendelea kukua 2016 , lakini changamoto bado zipo:

Ukuaji wa uchumi barani Afrika unatarajiwa kupanda na kufikia asilimia 4.2 mwaka 2016 baada ya mambo kutokuwa mazuri sa na mwaka uliopita.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya matazamo wa uchumi wa duniani iliyochapishwa na benki ya dunia mwezi huu ,ambayo pia inasema kwa ujumla uchumi unatarajiwa kukua kote duniani chini ya asilimia 3.

Marc Stocker ni afisa uchumi kwenye Benki ya Dunia na ni miongoni mwa waandishi wa ripoti hiyo, anasema japo uchumi utaendelea kukua Afrika kuna baadhi ya nchi zinakabiliwa na changamoto kubwa.

(SAUTI YA MARC STOCKER)

"Kuna tofauti katika ukanda ukiangalia uchumi wa nchi tatu tofauti ikiwemo Nigeria, Afrika Kusini na Angola, nchi tatu hizi zitaendelea kukabiliwa na changamoto, Nigeria ikikabiliwa na uhaba wa umeme na mafuta, uimarishaji wa fedha, usimamizi wa fedha za kigeni na Afrika Kusini kuna shida ya umeme, matatizo ya mahusiano ya kazi na kutokuwepo na uhakika wa kisiasa, na Angola matumizi ya serikali yanapunguzwa na mfumko wa bei unaoathiri ununuzi. Kwa hiyo Uchumi wa nchi hizi utaendelea kukabiliwa na changamoto."